Klabu ya soka ya Manchester United imetangaza mapato yao ya robo ya Kwanza ya Mwaka wa Kifedha.
Mapato ya Man United kwa Miezi Mitatu, iliyoiishia Septemba, ni Pauni Milioni 123.6 ikiwa ni ongezeko la Asilimia 39 kwa kipindi kama hiki kwa Mwaka 2014.
Pia mapato yameongezeka baada ya kusaini Mkataba mpya na kampuni ya vifaa vya michezo vya Adidas ambayo yatawaingizia Pauni Milioni 750 kwa Miaka 10 ukiwa ni Mkataba mkubwa kabisa Duniani kwa Klabu na Watengeneza Vifaa vya Michezo.
Vilevile, kushiriki kwa timu hiyo katika michuano ya Uefa Championz ligi kumechangia ongezeko la pato lao kwenye Matangazo ya Mechi kwa Asilimia 64.3.
Asilimia 64.2 hutokana na vingilio vya mashabiki pamoja na kuuzwa kwa bidhaa nyingine zikiwemo jezi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni