Mchezaji wa Stoke City Ryan
Shawcross ameahidiwa manukato ya kumtosha mwaka mmoja baada ya
mshambuliaji wa Chelsea Diego Costa kuonekana kutofurahishwa na harufu
ya mwili wake.
Costa alionekana kunusa makwapa yake mwenyewe na kisha kumuelekezea kidole Shawcross kabla ya kujishika pua.
"Tumehakikisha Ryan Shawcross anajipaka marashi yake jioni hii," mkewe difenda huyo wa umri wa miaka 28, Kath aliandika kwenye Twitter baada ya mechi hiyo.
Shawcross alijiunga na meneja wa klabu hiyo Mark Hughes katika mkutano wa mashabiki wa Stoke ambako alikabidhiwa marashi hayo ya kumtosha mwaka mmoja.
"Costa alipokuwa akiniangazia badala ya kuangazia mechi, sisi tulijishindia mechi,” Shawcross aliambia mkutano huo.
"Yeye ni mchezaji nyota sana na nina furaha kwamba nilimnyamazisha.”
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni