Na Boniface Wambura, Dar es salaam
Timu
ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 (Serengeti Boyz)
inacheza mechi ya kujipima nguvu kesho (Julai 11 mwaka huu) dhidi ya
Azam U-20 kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.
Mechi
hiyo ambayo ni maalumu kwa benchi la ufundi la Serengeti Boyz
likiongozwa na kocha Hababuu Ali Omari kuangalia kikosi chao itaanza saa
2 kamili asubuhi.
Serengeti
Boyz itacheza mechi yake ya kwanza ya raundi ya pili ya michuano ya
Afrika dhidi ya Afrika Kusini (Amajimbos) siku ya Ijumaa, Julai 18 mwaka
huu kwenye uwanja huo huo wa Azam Complex kuanzia saa 10 kamili jioni.
Wachezaji
wanaounda kikosi cha Serengeti Boyz ni Abdallah Shimba, Abdulrasul
Bitebo, Abutwalibu Mshery, Adolf Bitegeko, Ally Mabuyu, Ally Mnasi, Amin
Noren, Athanas Mdamu, Badru Othman, Baraka Baraka, Hatibu Munishi na
Issa Athuman.
Wengine
ni Juma Yusuf, Kelvin Faru, Kelvin Kamalamo, Martin Luseke, Mashaka
Ngajilo, Mechata Mnata, Mohamed Abdallah, Mussa Vicent, Nazir Barugire,
Omary Omary, Omary Wayne, Prosper Mushi, Seif Seif na Yahya Hafidh.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni