Anakwenda Anfield? Divock Origi (kulia) amesafiri mpaka Liverpool kujadili uwezekano wa kujiunga na klabu hiyo.
Liverpool wanakaribia kukamilisha usajili wa wachezaji wawili, nyota wa Ubelgiji katika fainali za kombe la dunia mwaka huu, Divock Origi na winga wa Benfica, Lazar Markovic.
Usajili huo utaigharimu Liverpool dau la paundi milioni 30.
Orig alipigwa picha akiwasili mjini
Liverpool jana jumatano ili kuzungumza na maofisa wa klabu katika
uwanjani wa mazoezi wa Melwood na anaweza kupimwa afya leo alhamisi.
Ada ya uhamisho ya paundi milioni 19.8
kwa ajili ya Markovic inaaminika imeshakubaliwa na Benfica, wakati Origi
anaonekana ataigharimu Liverpool paundi milioni 10 kutokea klabu ya
Lille ya Ufaransa,.
Hata hivyo, nao Tottenham waliripotiwa kuiwinda saini ya nyota huyo.
Akiwasili: Origi (pichani mwenye nguo yenye rangi ya njano) alichukuliwa kwenda uwanja wa mazoezi wa Liverpool, Melwood
Mambo bado: Japokuwa Origi aliwasili Merseyside dili baod halijakamilika
Origi aliyeichezea Lille msimu uliopita anaivutia Tottenham
Kocha Brendan Rodgers anatarajia
kutumia paundi milioni 75 atakazopata kwa kumuuza Luis Suarez katika
klabu ya Barcelona na anakaribia kumuongeza Markovic kikosini.
Klabu hiyo ya Anfield imekuwa katika mazungumzo na Benfika kwa wiki kadhaa ili kuinasa saini ya nyota huyo mwenye miaka 20.
Markovic ameichezea Serbia mechi 12,
akifunga mabao mawili na alifunga mabao 49 katika mechi alizoichezea
Benfica msimu uliopita.
Origi amegeuka kuwa mvuto baada ya
kung`ara katika fainali za kombe la dunia mwaka huu nchini Brazil,
akifunga bao katika hatua ya makundi dhidi ya Urusi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni