Gwiji: Mourinho (kushoto alimleta Drogba katika klabu ya Chelsea mwaka 2004 akitokea Marseille ya Ufaransa.
Nyota huyo mwenye miaka 36 anazivutia
klabu za Qatar, wakati Juventus nao wakifikiria kumnasa mkongwe huyo
anayecheza katika klabu ya Galatasaray ya Uturuki.
Bado Jose Mourinho ana mahusiano mazuri na Muivory coast huyo na anavutiwa kumrudisha kwa majukumu ya ukocha zaidi.
Mkongwe huyu wa miaka 36 anazivutia klabu za Qatar, nao Juventus wanaitaka saini yake.
Klabu hizo za Qatar zinatarajia kutoa
ofa nono na mshahara utajadiliwa, lakini unakadiriwa kuwa paundi milioni
3 kwa msimu baada ya makato ya kodi.
Wazo la kurudi Chelsea litaangaliwa zaidi na pande zote.
Mourinho amekuwa na mapenzi makubwa kwa Drogba na anajua kuwa atakuwa na msaada mkubwa katika kikosi chake msimu ujao.
Alionesha nia hiyo hata Galatasaray
ilipokutana na Chelsea katika michuano ya UEFA mwezi machi mwaka huu na
alieleza kuwa Drogba anaweza kurudi na yuko makini kufanikisha hilo.
Drogba alishinda makombe matatu ya ligi,
makombe manne ya FA na kombe la UEFA akiwa katika klabu ya Chelsea na
Mourinho anataka kutumia uzoefu wake kuwashauri wachezaji wake wapya.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni