Shirikisho la soka Duniani, FIFA limetangaza kwamba uchaguzi
mkuu wa Rais utafanyika Februari 26 mwakani.
Maamuzi haya yamefanyika leo katika kikao cha kamati ya
utendaji ya Shirikisho hilo kilichofanyika mjini Zurich, Uswisi.
Sepp Blatter aliyejiuzulu siku nne baada ya kuchaguliwa
amethibitisha kuwa ataendelea kukaa madarakani mpaka uchaguzi mkuu utapofanyika
kupata mrithi wake.
Wakati huo, kundi la watu wanaoshinikiza kufanyika kwa mageuzi wamekutana leo mjini
humo wakimuomba katibu mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa, Kofi Annan kuongoza
mapinduzi hayo.
Kundi hilo limesema Annan ni mtu makini ambaye anapaswa
kuongoza tume ya mageuzi wakati huu
Dunia ikielekea kupata mrithi wa Sepp Blatter aliyejiuzulu Urais kutokana na
kashfa nzito ya rushwa iliyokumba FIFA.
Shirika la Ujasusi la Marekani, FBI liliwatia mbaroni
Maafisa saba wa ngazi za juu wa FIFA kwa tuhuma za rushwa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni