Bastian
Schweinsteiger amemuelezea mchezaji mwenza wa Manchester United Memphis
Depay kama "kipaji kisichoelezeka", baada ya kumuona katika mchezo wake
wa kwanza kwenye mechi maandalizi ya msimu mpya wa ligi.
Kiungo
huyo wa kimataifa wa Ujerumani, ambaye amesajiliwa kutoka Bayern Munich
kwa kitita cha pauni milioni 14, aliingia kipindi cha pili katika
mchezo dhidi ya Club America na kuisaidia timu yake kuibuka na ushindi
wa goli 1-0 katika dimba la CenturyLink.
Akiongea
na tovuti ya klabu baada ya ushindi huo, Mjerumani huyo amesema kuwa
ana imani kubwa mashabiki wa klabu hiyo wafaidi makubwa kutoka kwa
Depay.
"Memphis
ni kipaji kisichoelezeka na ana ubora wa hali ya juu na nina uhakika
tutafurahia sana atakachokuwa akikifanya uwanjani pindi msimu
utakapoanza", alisema.
"Nimefurahi
sana kwa sababu kuwaangalia vijana namna wanavyocheza kwa mfano
[Andreas] Pereira, Jesse [Lingard] na [James] Wilson. Wote ni wachezaji
wazuri.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni