STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumatatu, 13 Julai 2015

KUMBUKUMBU KUBWA MICHEZONI SIKU KAMA YA LEO... NI NOUMA SANA

kikosi cha Marekani kilichoshiriki mashindani ya kwanza ya kombe la dunia 1930 nchini Uruguay na kushinda mchezo wa kwanza dhidi ya Ubelgiji.

Wakati soka likiwa na mengi ya kukumbuka. Leo ikiwa ni Julai 13 mwaka 2015, yapo mengi yalipata kujiri tarehe kama ya leo miaka kadhaa iliyopita.
Julai 13 mwaka 1930, ilikuwa ni siku ambayo kwa mara ya kwanza mashindano ya kombe la Dunia yalikuwa yanafunguliwa nchini Uruguay kwa michezo miwili ambapo timu ya taifa ya Ufaransa iliiadhibu Mexico mabao 4-1 huku Marekani wakiibuka na ushindi wa 3-0 dhidi ya Ubelgiji katika michezo hiyo ya ufunguzi iliyopigwa mji mkuu wa Uruguay, Montevideo.
Fainali hizo ziliisha kwa wenyeji Uruguay kuibuka machampioni kwa kuifunga Argentina 4-2 katika mchezo wa fainali ambao ulikuwa ni kama marudio ya mchezo wa fainali ya Olympic ya mwaka 1928.
aliyewahi kuwa kocha wa timu ya taifa ya Italia (2006-2008), Roberto Donadoni
Ukiachana na hilo, tarehe kama ya leo mwaka 2006, ni siku ambayo Italia walimtangaza rasmi kiungo wa zamani wa AC Milan, Roberto Donadoni anayekumbukwa kwa kushinda mataji 6 ya Italia akiwa na Milan pamoja na mataji 3 ya Ulaya kama kocha mkuu wa timu ya taifa hilo akichukua pahala palipoachwa na Marcelo Lippi aliyeamua kusepa baada ya kuiwezesha Italia Kutwaa kombe la dunia katika fainali zilizofanyika mwaka huo nchini Ujerumani mwaka huo.
kutoka kulia (Antonio Valencia, Sir Alex Ferguson, Michael Owen na Gabriel Obertan) baada ya kukamilisha usajili wao Man Utd Julai 13 mwaka 2009.
Mashabiki wa Manchester United watakuwa wanaikumbuka sana siku hii kwani mnamo siku kama ya leo mwaka 2009, Sir Alex Ferguson alikamilisha usajili wa nyota watatu kwa mpigo ambao ni Gabriel Antoine Obertan, Michael James Owen na Luis Antonio Valencia. Wachezaji ambao walikuwa na mchango mkubwa kila mmoja kwa nafasi yake na kuiwezesha United kutwaa ubingwa wa Uingereza msimu wa 2010/11 baada ya kuupoteza kwa Chelsea msimu wa 2009/10. Antonio Valencia ndiye mchezaji pekee aliyedumu hadi sasa katika kikosi cha mashetani hao wekundu baada ya wenzake wawili (Owen na Obertan) kuuzwa.
Bastian Schweinsteiger akiwa na kombe la Dunia baada ya kushinda taji hilo na Ujerumani Julai 13 mwaka 2014.
Kingine cha kufurahisha ni kuwa mnamo tarehe kama ya leo (Julai 13) lakini mwaka 2014, kiungo wa kimataifa wa Ujerumani Bastian Schweinsteiger alishinda taji la kombe la Dunia akiwa na Ujerumani wakiifunga Argentina katika mchezo wa fainali kwa goli pekee la kiungo aliyekuwa akikipiga naye Bayern, Mario Gotze. 
Kizuri ni kuwa hii ni Siku ambayo bado inazidi kuwa na maana kubwa kwake katika maisha yake ya soka kwani tarehe kama hiyo mwaka 2015 amekamilisha usajili wake rasmi kuelekea Manchester United akimaliza kipindi chake cha kuwatumikia ‘Mabavaria’ Bayern Munich.
Bastian Schweinsteiger (kulia) akiwa na Louis Van Gaal zama za utawala wake Bayern Munich.
Kwa kuwa tunathamini kumbukumbu, Haya ni machache kati ya mengi yanayohusu soka unayoweza kukumbuka yaliojiri tarehe kama ya leo lakini miaka kadha iliyopita.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox