Manchester
United imetangaza kikosi kinachoenda katika ziara ya maandalizi ya
msimu mpya 'pre-season tour party' nchini Marekani na Stori kubwa ni kuchaguliwa kwa golikipa wa mashetani hao wekundu, David De Gea.
Licha
ya muendelezo wa tetesi za kutimka Old Trafford kwenda Real Madrid
majira haya ya kiangazi, De Gea mwenye miaka 24 amejumuishwa kwenye
kikosi hicho, huku Golikipa namba mbili wa United, Victor Valdes akiachwa kwenye orodha hiyo.
Kukosekana kwa Valdes kumewashangaza wengi na kuongeza tetesi kwamba anaweza kuondoka klabuni hapo.
Wachezaji wapya waliosajiliwa Memphis Depay, Morgan Schneiderlin, Matteo Darmian na Bastian Schweinsteiger wamejumuishwa pia.
Wachezaji wengine walioachwa kwenye kikosi ni Angel Di Maria na Marcos Rojo (ambao wote walicheza Copa America). Pia mlinzi wa kulia Rafael ameachwa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni