Josep
Maria Bartomeu amechaguliwa tena kuwa raisi wa Barcelona kwa muhula wa
pili, akimshinda Joan Laporta ambaye ameshawahi kuwa raisi wa klabu
hiyo.
Taarifa
kutoka kituo cha habari cha Barcelona kinasema kwamba Bartomeu alipata
kura asilimia 54.63 ambazo zilipigwa jana Jumamosi.
Bartomeu kwa ushindi huo ina maana ataiongoza klabu ya Barcelona kwa miaka sita mingine.
Bartomeu
alipata kiti cha uraisi baada ya raisi aliyekuwa mwanzo Sandro Rosell
kujiuzulu kufuatia shutuma zilizokuwa zinamkabili juu ya usajili wa
Neymar kutoka Santos.
Bartomeu
akiwa amefanikia kuisimamia Barcelona kupata ubingwa wa Copa del Rey,
La Liga na Klabu Bingwa Ulaya aliweza kumshinda mpinzani wake Joan
Laporta ambaye aliongoza klabu hiyo kuanzia 2003 mpaka 2010
MGAWANYO WA KURA;
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni