Ukiwafuatilia makocha wengi Duniani, hupendelea kuwafundisha
wachezaji kupiga penalti upande wa pembeni wa goli kuliko katikati.
Mpira ukipigwa pembeni ya goli una asilimia kubwa ya kuingia kwa sababu ya kasi au Golikipa kuchelewa kufika, lakini katikati ni kama kuchezea shilingi chooni.
Kwa vile wachezaji wengine wana kiburi kutokana na uzoefu wao pamoja na utaalam, huamua kuleta vionjo katika upigaji wa penalti ingawa utundu huu unaweza kumfanya awe Shujaa au ziro kabisa.
Moja ya wanasoka wenye kiburi cha kupiga penalti za vionjo ni kiungo wa zamani wa Juventus, Andrea Pirlo ambaye hupendelea kupiga penalti aina ya panenka.
Aina hii ya penalti hupigwa katikati ya goli na kipa huhama upande wa kulia au kushoto, huku mpira ukipita katikati kwa juu. Panenka ni penalti ambayo inakuweka katikati ya ushujaa na u-ziro.
Mwanzilishi wa penati hii ni kiungo mshambuliaji wa Czechoslovakia mzaliwa wa Prague Antonin Panenka alifunga stahili hiyo ya penati mwaka 1976 katika kombe la mataifa bingwa barani ulaya kwenye hatua ya fainal dhidi ya Ujerumani Magharibi.
Ilikuwa ni penati ya ushindi kwa Czechoslovakia baada ya mshambuliaji wa Ujerumani Ulrich Hoeneß kukosa mkwaju wake wa penati na ndipo Panenka akafanikwa kufunga penati ambayo iliwezesha taifa lake kuibuka na ushindi
wa penati 5-3 apo awali timu zote zilifungana 2-2 kwenye muda wa kawaida.
Baada ya kufunga penati hiyo ikatambuliwa kama "Panenka staili" wapo wachezaji wengi ambao hujaribu kupiga staili hii ya penati ambapo ni wachache sana hufanikiwa kufunga kama kina Gonzalo Pineda,Zinedine Zidane,Sebastián Abreu,Lionel Messi,Alexis Sanchez,Francesco Totti hao ni baadhi tu waliofanikiwa kufunga staili hii.
Nahodha wa Yanga, Nadir Haroub 'Cannavaro' aliwahi kupiga panenka dhidi ya Al Ahly ya Misri katika mechi ya ligi ya mabingwa barani Afrika iliyopigwa mjini Alexandria, Misri, Yanga wakitolewa kwa matuta.
Cannavaro alionekana shujaa, alishangiliwa mno, lakini jana amejaribu kupiga panenka dhidi ya Gor Mahia na kuchemsha.
Wapo pia wachezaji mbalimbali walio chemka kufunga penati kwa staili hii ya mkongwe Panenka Neymar,Antonio Cassano,Alexandre Pato na Robin van Persie na wengine wengi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni