Robin
van Persie amejibu mapigo kwa kocha wake wa zamani Louis van Gaal,
baada ya kutompa nafasi ya kuthibitisha utayari wake kwa ajili ya
mapambano mapya katika klabu ya Manchester United.
“Hiyo ilikuwa ni ishara ya kwanza kwamba mambo yalikuwa hayaendi kama ilivyotakiwa”, aliliambia gazeti la the Sunday Times.
“Nilimuomba
kucheza nikitokea benchi, ili nirudishe kasi yangu ya awali, lakini
baada ya hapo niliendelea kuwekwa bechi tena. Hali ilibadilika kati
yangu na Louis na hata baadhi ya watu kwenye timu waliona hilo, lakini
mara zote nilikuwa mweledi. kwa wakati huo sikuwa nimefikiria kuondoka.
[Mke wa Van Persie] Bouchra alikuwa na furaha tu. watoto walikuwa na
furaha katika jiji la Manchester.
“Lakini
hata hivyo bado nilikuwa na fikra ya kwamba nikirudi kutoka mapumzikoni
tutaanza mambo upya. Alikwisha badili maamuzi yake kuhusu mimi tangu
hapo kabla. Wakati alipoanza kuifundisha Uholanzi aliwahi kuniambia
kwamba‘Wewe ni mshambuliaji chaguo la tatu hapa.’ Nikasema sio tatizo’
Lakini nilipambana na baadaye kuwa chaguo la kwanza na nahodha wake pia.
“Lakini
wakati niliporudi, Hakukuwa na uhalisia wa kile kilichokuwa
kikiendelea. Kupambana ili kurejea katika kikosi cha kwanza haikuwa ombi
bali ni lazima kwangu. Alinipeleka kwenye kikosi cha pili. Na mimi ni
mchezaji niliyekwisha pevuka tayari. Sio mpuuzi mimi. Kamwe siku na
hasira wala jazba.
Haya mambo ni sehemu ya mchezo, sehemu ya maisha.
lazima ufanye maamuzi sahihi katika wakati wowote ule, hivyo basi
nafanya hili ili nisonge mbele.
“Namjua Louis kama kocha wa timu ya taifa na sasa namjua kama kocha wa klabu. N awkati huo huo kumbe kuna utaofauti mkubwa”.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni