Hatimaye kiungo
wa Southampton, Morgan Schneiderlin amekamilisha vipimo tayari kujiunga na Manchester
United wiki hii.
Schneiderlin
ambaye alikua akiwaniwa na klabu za Arsenal, Manchester United na Tottenham
Hotspur, amefikia tamati baada ya kutua Carrington uwanja wa mazoezi wa United,
kufanyiwa vipimo tayari kwa kuuvaa uzi wa klabu hiyo.
Schneiderlin
mwenye miaka 25 alikua kiungo wa pili nyuma ya kiungo wa Chelsea, Nemanja Matic
kwa 'tackling' nyingi msimu uliopita.
Morgan
Schneiderlin, raia wa Ufaransa atakua ametimiza ndoto zake za kucheza klabu
bingwa Ulaya, kwani ndicho kilichomuondoa Soton.
Awali Southampton
walikataa ofa ya pauni 20m kutoka kwa Manchester United, kwa kuwa wanaamini
thamani ya kiungo huyo mkabaji ni zaidi ya pauni 25m.
Aidha huo ni
usajili wa nne wa klabu hiyo ya Manchester msimu huu mara baada ya kuwanasa
tayari, Memphis Depay, Matteu Darmian na Bastian Schweinsteiger.
Wakati huo
huo imeelezwa kuwa bado Manchester United inasaka saini ya mlinzi wa Real
Madrid, Sergio Ramos ili wakamilishe usajili wao
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni