Ofa
iliyokubaliwa ya Manchester City kumsajili kiungo Raheem Sterling
kutoka klabu ya Liverpool imeweka rekodi mpya katika orodha ya wachezaji
ghali zaidi wenye asili ya taifa la Uingereza.
Man
City wamekubali kuilipa Liverpool ada ya kiasi cha paundi milioni 49
kwa ajili ya kumnasa Sterling na kumfanya kuwa mchezaji ghali zaidi
ambaye bado yupo chini ya umri wa miaka 21.
Raheem
Sterling sasa anashika nafasi ya pili nyuma ya Gareth Bale aliyeuzwa
miaka miwili iliyopita kwa ada iliyovunja rekodi ya Dunia ya paundi
millioni 85.3 – akitokea Tottenham kwenda Madrid.
Andy Carrol anashika nafasi ya 3 kwa kuuzwa kiasi cha paundi millioni 35 akitokea Newcastle kwenda Liverpool.
Rio
Ferdinand alinunuliwa na Manchester United akitokea Leeds United kwa
Paundi milioni 30 na kuweka rekodi ya kuwa beki ghali zaidi kuwahi
kutokea kwa kipindi hicho.
ORODHA KAMILI HII HAPA::
1-Paundi milioni 85.3 – Gareth Bale (Tottenham kwenda Real Madrid, 2013)
2-Paundi milioni 49* – Raheem Sterling (Liverpool kwenda Manchester City, 2015) * uhamisho bado haujakamilika lakini.
3-Paundi Milioni 35 – Andy Carroll (Newcastle kwenda Liverpool, 2011)
4-Paundi milioni 30 – Rio Ferdinand (Leeds kwenda Manchester United, 2002)
5-Paundi milioni 27 – Luke Shaw (Southampton kwenda Manchester United, 2015)
Sawa na Wayne Rooney Paundi milioni 27 – (Everton kwenda Manchester United, 2004)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni