Roberto
Mancini amekiri kwamba alikuwa akimuonea wivu Jose Mourinho kushinda
makombe matatu wakati alipokuwa akiifundisha Inter na kuongeza kuwa
amefanya maamuzi ya kipuuzi kurudi kuifundisha klabu hiyo kwa mara
nyingine tena.
Licha
ya kushinda kombe la ligi kuu nchini humo mara tatu mfululizo katika
kipindi chake cha mwanzo, Muitaliano huyo alifukuzwa na nafasi yake
kuchukuliwa na Jose Mourinho katika msimu wa majira ya joto wa mwaka
2008.
“Sikutarajia kufukuzwa”, Mancini aliiambia Gazzetta TV.
“Nilisoma
habari kutoka katika gazeti moja asubuhi ya siku hiyo, na wasiwasi
fulani hivi ukanijia. Massimo Moratti aliniita na kuniambia kwamba yale
ndio maamuzi aliyochukua.
“Alimtaja
Mourinho? Hapana. Sio mbaya acha tu nimshukuru Moratti, kwa sabbabu
alinipa fursa ya kuwa kocha wa Inter kwenye wakati ambao ulikuwa ni
muhimu sana katika maisha yangu”.
Alipoulizwa
kuhusu Mourinho, Mancini alijibu: “Nadhani ni kocha mzuri. Je nina wivu
juu ya makombe matatu? Hizi ni fikra zilizopo ndani, lakini naamini
vitu hivi vilitokea kwa sababu vilipangwa kutokea”
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni