Mtanzania
anayecheza mchezo wa mpira wa kikapu nchini Marekani Hasheem Thabeet
ametolewa uwanjani baada ya kufanya madhambi mara mbili.
Hasheem
anapambana kwa sasa ili kuweza kurejesha ndoto zake za kucheza ligi kuu
ya NBA, lakini amekua akipokea ushauri kutoka kwa wadau wa mchezo huo
wa kumtaka kuelekeza fikra zake katika nchi nyingine kutokana na umri
kumtupa mkono.
Hasheem alifanya madhambi mara mbili katika mchezo wa D League, ambao ulishuhudia kikosi cha Washington Wizards kikipambana.
Mwamuzi
wa mchezo huo alionyesha ishara kwa mchezaji huyo, kwa kuujulisha umma
uliokua unashuhudia mpambano huo ni vipi alivyofanya makosa ambayo
yalistahili kumpeleka nje ya uwanja.
Mdau
wa michezo nchini Marekani, Chris Vivlamore aliandika katika ukurasa
wake wa Twitter, sekunde chache mara baada ya Hasheem kuamuriwa kutoka
nje ya uwanja maandishi ambayo yalionekana kama kejeli kwa mchezaji huyo
wa kibongo.
Aliandika
“Hasheem Thabeet, anayecheza D-League, amefanya madhambi mara mbili na
kutolewa nje ya uwanja, na sasa yupo kwenye vyumba vya kubadilishia
akipiga mabenchi pamoja na locker (Makabati).”
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni