Golikipa
Hugo Lloris wa klabu ya Tottenham Hotspur ya jijini London, ameipa pigo klabu
yake ya Spurs baada ya kuumia katika mazoezi ya kujiandaa na msimu mpya wa ligi
kuu England.
Nahodha huyo
wa Tottenham Hotspur amevunjika mifupa ya kiganja cha mkono katika mazoezi ya awali
na 'preseason' na klabu yake.
Golikipa huyo
raia wa ufaransa, anatarajiwa kuukosa mchezo wa kwanza wa ligi dhidi ya Manchester
United katika uwanja wa Old Trafford mwezi ujao wa Agosti.
Pamoja na
kuwa ni pigo kwa Spurs lakini taarifa hizi sio pia nzuri kwa Manchester United
ambao wanawania saini ya mlinda mlango huyu hasa kutokana na kutokuwa na uhakika
wa mustakabali wa kipa wao David de Gea anayewindwa na Real Madrid.
Katika hali
ya sintofahamu, golikipa De Gea amejumuishwa katika safari ya preseason na
wenzake nchini Marekani huku fukuto la kutakiwa na Madrid likiwa linaendelea
chinichini.
Aidha
golikipa mwenza wa Manchester United, Victor Valdez ameachwa katika safari hiyo
bila ya taarifa zozote kutolewa. Hali hiyo inatokea wakati klabu za nchini
Uturuki zikimwania Valdez ambaye alitamba na klabu ya Barcelona kwa misimu 13
kabla ya kuumia na kisha kuondoka akiwa huru.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni