ZOEZI
la usajili kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Bara linaendelea kwa
sasa nchini na limewanufaisha baadhi ya wachezaji ambao kwa namna moja
au nyingine, wala hawakuota kuangukiwa na zali.
Wapo baadhi ya wachezaji hawakuota kama wangekuja kucheza michuano ya
Kombe la Kagame, lakini ni usajili unaoendelea ndio umewapa zali hilo.
Wachezaji hao kama wangebaki katika klabu zao ingekuwa vigumu kwao
kuicheza michuano hiyo inayoshirikisha Klabu Bingwa Afrika Mashariki na
Kati itakayoanza mwishoni mwa wiki hii jijini Dar es Salaam. Hii ni kwa
sababu klabu zao hazina sifa za kushiriki michuano hiyo.
Ifuatayo ni orodha ya wachezaji wachache walioangukiwa na bahati ya kuicheza michuano hiyo ya mwaka huu bila kutarajia.
Ramadhani Singano-Azam
Ametua
Azam FC wakati ikijiandaa na michuano ya Kagame, hivyo ni wakati mzuri
kwake kujaribu bahati yake ya kuonyesha kiwango kwa timu za nje.
Wakati
mwingine mgogoro wake na timu yake ya zamani Simba, umemsaidia yeye
kumpa hatua nyingine, ni wazi kama angekuwa katika klabu yake ya zamani
basi angekuwa mtazamaji kwani Simba haishiriki michuano hiyo kwa miaka
mitatu sasa.
Malimi Busungu-Yanga
Ni
lazima amshukuru Mungu kwa kusajiliwa kwake Yanga ambayo imepata nafasi
ya kushirikiki Kagame kwani angekuwa Mgambo JKT, timu yake ya zamani
basi angekuwa anaisikia michuano hiyo hewani ama wakati mwingine
angekuwa anatazama wenzake wakifanya kazi.
Akiitumia
vyema nafasi atakayopata Yanga, basi ni dhahiri ndoto yake inaweza
kupenya umbali mrefu hasa kwa timu zinazoshiriki michuano hiyo.
Geofrey Mwashiuya
Kweli
mwenye bahati habahatishi kwani ni adimu sana mchezaji kung’ara kutoka
timu ya Ligi Daraja la Kwanza kisha akatikisa kwenye klabu kongwe kama
Yanga, haikuwa rahisi kwake kuwa mmoja wa wachezaji wanaotarajiwa
kucheza Kagame.
Mchezaji
huyo kutoka Kimondo ya Mbozi, ametua Jangwani na mguu wa bahati kwani
ameingia Yanga wakati ikijiandaa na michuano hiyo na ni muda mwafaka
kwake kuonyesha uwezo wake katika michuano hiyo ya Kagame.
Deus Kaseke-Yanga
Amebahatika
kusajiliwa Yanga ambayo inashiriki michuano ya Kagame inayotarajiwa
kuanza Jumamosi na kikosi chake kitafungua pazia la michuano hiyo dhidi
ya Gor Mahia ya Kenya.
Kiwango
chake ndicho kilichomchomoa Mbeya City ambayo haipo kwenye michuano
hiyo ingawa wadau wengi walitarajia huenda ingeshiriki kutokana na
Tanzania Bara kuwa wenyeji hivyo walitarajia wangetoa timu tatu nayo
ingekuwepo. Kama angeamua kuongeza mkataba Mbeya City ni wazi ingekula
kwake na asingepata bahati ya kushiriki michuano hiyo.
Ame Ali-Azam
Wenyewe wanamwita Zungu. Alikuwa Mtibwa Sugar ambayo ilianza Ligi Kuu msimu uliopita kwa mkwara kabla ya kutepeta.
Kama
angesalia katika timu hiyo ya Wakata Miwa, ni wazi asingepata nafasi ya
kuuza sura Kagame, lakini kusajiliwa kwake na Azam kunampa uhakika wa
kulitangaza jina lake kama atafanya mambo makubwa.
Kutua kwake Azam, kunampa Zungu nafasi ya kufanya yake akishirikiana na wachezaji wenzake chini ya kocha Stewart Hall.
Zungu
ni bonge la mchezaji na kama asingepata nafasi hiyo ndani ya Azam,
angekuwa mtazamaji wa kuwaangalia wenzake wakifanya yao kwa raha zao.
Haya tusubiri tuwaone uwanjani.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni