MASHABIKI
wa Leeds United wamepewa mkong'oto na mashabiki wa Eintracht Frankfurt
usiku wa jana baada ya mchezo wa kirafiki baina ya timu hizo
uliofanyika Austria.
Polisi
mjini humo wamewashutumu mashabiki wa timu ya Ujerumani kwa kuanzisha
vurugu, ambazo zilisababisha watu 25 wakamatwe na wengine kibao kuachwa
wanavuja damu kwa majeraha.
Taarifa
kutoka katika eneo la tukio, zinasema kwamba kundi la mashabiki 100 wa
Frankfurt baadhi yao wakiwa wamevaa vitu vya kuficha sura zao,
liliwavamia kundi la mashabiki wa Leeds uwanjani baada ya Wajerumani
kushinda 2-1.
Mara tu baada ya mechi mashabiki wa timu hizo walianza kutupiana makonde na mateke uwanjani mjini Eugendorf, karibu na Salzburg.
Mashabiki
watatu wa Leeds, Maofisa wawili wa Polisi na walinzi wa uwanjani
walipelekwa hospitali kwa matibabu. Inaaminika kwamba 17 kati ya
waliokamatwa walikuwa mashabiki wa Frankfurt.
Polisi ilitumia mabomu na mbwa kuwatawanya mashabiki hao waliokuwa katikati ya mpambano mkali.
Shabiki huyu wa Leeds United alikuwa mkong’oto wa nguvu na kuvuja damu
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni