UEFA
imetoa orodha ya wachezaji ambao wanawania tuzo ya mchezaji bora wa
Ulaya kwa mwaka 2015. Majina ya wachezaji waliocheza fainali ya UEFA
Champions League kati ya Barcelona dhidi ya Juventus yametawala kwenye
orodha hiyo huku Lionel Messi na Paul Pogba wakipewa nafasi ya juu
kutwaa tuzo hiyo.
Winga
wa Chelsea Eden Hazard pia ameingia kwenye orodha hiyo akiwa ni
mchezaji pekee kutoka kwenye ligi ya England ambaye anapambana na wakali
wengine kutoka La Liga na Serie A. Tovuti rasmi ya UEFA imetoa taarifa
zaidi juu ya listi hiyo inayomjumuisha pia mshambuliaji wa Real Madrid
Cristiano Ronaldo.
Ladha
ya Barca-Juve imekuja bila kipingamizi. Miamba ya Catalan iliyoshinda
vikombe vitatu msimu uliopita kwa kusaidiwa na washambuliaji watatu
waliopewa jina la ‘utatu mtakatiu’ unaoundwa na Messi, Luis Suarez
pamoja na Neymar ambao wote wapo kwenye orodha hiyo.
UEFA 2015
Wakati
Juve wakitumaini kutwaa taji lao la tatu msimu huu waliangukia pua
mbele ya Barca lakini bado Andrea Pirlo na Arturo Vidal wanaungana na
Pogma kwenye orodha hiyo.
Wachezaji
ambao walidhaniwa wangeinia kwenye orodha hiyo lakini wamepigwa chini
ni pamoja na mshambuliaji wa Sevilla Carlos Bacca na winga wa Arsenal
Alexis Sanchez. Bacca aliifungia Sevilla magoli 28 pamoja na kuisaidia
timu hiyo kushinda taji la Europa League.
Wakati
Sanchez yeye alifunga magoli 25 na kuisaidia Arsenal kutwaa taji la FA
lakini kuenguliwa kwao kwenye orodha hiyo kumezua maswali mengi.
Watu
wameanza kutabiri kuwa, mshindi wa tuzo hiyo atakuwa ni miongoni mwa
wachezaji waliocheza fainali ya Champions League msimu uliopita huku
Messi akipewa nafasi kubwa pamoja washambuliaji wenzie kutoka Barcelona.
Agosti 12 watatangazwa wachezaji walioingia tatu bora wakari msindi atatangazwa Agosti 28 Monaco, Ufaransa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni