KIPYENGA
cha michuano ya 40 ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la
Kagame kinapulizwa leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kutakuwa
na mechi tatu katika siku ya kwanza leo kwenye viwanja viwili tofauti,
kwanza KMKM ya Zanzibar na Telecom ya Djibouti kuanzia Saa 8:00 mchana
na baadaye wenyeji Yanga SC dhidi ya Gor Mahia ya Kenya Saa 10:00 jioni
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, muda ambao pia APR ya Rwanda itamenyana
na Al Shandy ya Sudan Uwanja wa Karume.
Waziri
wa Ujenzi, Dk John Pombe Joseph Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi
katika ufunguzi wa michuano hiyo na mgombea huyo wa Urais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania (CCM) atawasili muda mfupi kabla ya mechi rasmi ya
ufunguzi wa Kagame ya 40 kuanza, kati ya Yanga na Gor.
Michuano
hiyo ina makundi matatu, A likijumuisha timu za Yanga SC, KMKM, Telecom
na Gor Mahia wakati wenyeji wengine, Azam FC wapo Kundi C pamoja na
Malakia ya Sudan Kusini, Adama City ya Ethiopia na KCCA ya Uganda na
Kundi B kuna APR ya Rwanda, Al-Shandy ya Sudan, LLB AFC ya Burundi na
Heegan FC ya Somalia.
Azam
FC itafungua dimba na KCCA Jumapili Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam Saa
10: 00 jioni mchezo utakaotanguliwa na mechi nyingine kati ya Adama City
na Malakia utakaonza Saa 8:00 mchana, wakati jioni Saa 10:00 Uwanja wa
Karume, LLB AFC itamenyana na Hegaan FC.
Mabingwa
wa michuano hiyo, El Merreikh ya Sudan hawakuja kutetea taji, kwa
sababu wapo kwenye hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Washindi
wa pili wa Ligi Kuu ya Sudan, El Hilal pia nao hawajaja kwa kuwa wapo
kwenye hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni