Kiungo wa Arsenal Aaron Ramsey amekiri kufurahishwa sana na taarifa za Barcelona kumtaka huku akisema kuwa angependa siku moja akacheze Uhispania.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Wales alikuwa akihusishwa na kuhamia Camp Nou mwanzoni kabisa mwa dirisha la usajili majira haya ya joto.
"Ni wazi kwamba ni jambo linalovutia kusikia hivyo", aliliambia Guardian".
"Barcelona walichukua makombe matatu msimu ulioisha na ni suala la luvutia mno kusikia unahusishwa na moja ya vilabu bora duniani."
"Siku moja ningependa kucheza nchini Uhispania na kupata uzoefu wa pale pia. Lakini kwa sasa nipo Arsenal na nina imani kubwa kwamba timu yangu itafanikiwa na kutoa changamoto kubwa kwa timu nyingine duniani.".
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni