Siku moja baada ya Shirikisho la soka Tanzania, TFF kutangaza kuvunja rasmi mkataba wa Ramadhan Singano 'Messi' na klabu yake ya Simba, winga huyo amesaini mkataba na Azam fc.
Messi amejiunga na Azam FC, imeelezwa ni mkataba wa miaka miwili.
Kujiunga kwake haraka Azam FC, kunaonyesha kweli Messi alikuwa amepania kuondoka Msimbazi iliyomkuza na kujiunga na Azam FC.
Ramadhani Singano anaanza kazi rasmi kesho ataungana na wenzake katika mazoezi ya Azam FC yanayofanyika chini ya
Mwingereza, Stewart Hall.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni