TANZANIA imezidi kuporomoka kwa kasi katika viwango vya ubora vinavyotolewa kila mwezi na Shirikisho la Soka Duniani-FIFA baada ya mwezi huu kushuka kwa nafasi 12.
Mwezi uliopita Tanzania iliporomoka kwa nafasi 20 kutoka nafasi ya 107 waliyokuwepo mpaka nafasi ya 127 na mwezi hali imeendelea kuwa hivyo kwani imeshuka mpaka nafasi ya 139.
Kwa upande wa nchi za Afrika Algeria wao ndio vinara wakiwa nafasi ya 19 duniani, wakifuatiwa na Ivory Coast waliopo nafasi ya 21, Ghana wako nafasi ya 25 huku Tunisia na Segegal wakikamilisha tano bora kwa kushinda nafasi ya 32 na 39.
Kwa upande wa Afrika Mashariki Uganda ndio wanaoongoza kwa kushika nafasi ya 19 kwa upande wa Afrika huku duniani wakishika nafasi ya 73, wanafuatiwa na Rwanda waliopo nafasi ya 20 kwa Afrika na Duniani 78.
Wengine ni Kenya walioko nafasi ya 34 kwa Afrika na 116 duniani, wakifuatiwa na Burundi waliopo nafasi ya 38 kwa Afrika na 131 duniani huku Tanzania tukishika mkia kwa ukanda huu kwa kuwa nafasi ya 42 kwa Afrika.
Mabingwa wa dunia Ujerumani wamenyofolewa katika nafasi ya kwanza kwenye orodha hizo ambayo imechukuliwa na Argentina wao wakiwa nafasi ya pili wakifuatiwa na Ubelgiji, Colombia na Uholanzi katika nafasi ya tatu, nne na tano.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni