KIUNGO
Bastian Schweinsteiger amekubali kujiunga na Manchester United kwa
Mkataba wa miaka mitatu, jambo ambalo ni habari njema kwa kocha Louis
van Gaal.
Inafahamika
kwamba uhusiano wa kiungo huyo wa Ujerumani na kocha Van Gaal umekuwa
sababu kubwa ya kukubali ofa ya United, ambayo inaaminika atakuwa
anapata mshahara wa Pauni Milioni 7.2 kwa mwaka katika miaka mitatu
ambayo ni sawa na maslahi yake ya sasa ya Bayern Munich.
Kwa mujibu wa gazeti la kila siku la Ujerumani, BILD,
mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 amewaambia mabosi wa Bayern
dhamira yake ya kuhamia United na yuko tayari kwenda Manchester
kufanyiwa vipimo vya afya na kusaini makaratasi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni