
TANZANIA
imetupwa nje ya michuano ya Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) baada
ya sare ya 1-1 jioni ya leo Uwanja wa Nakivubo, Kampala, Uganda.
Matokeo hayo yanamaanisha, Stars imetolewa kwa kipigo cha jumla cha mabao 4-1, baada ya awali kufungwa 3-0 katika mchezo wa kwanza wa Raundi hiyo ya kwanza visiwani Zanzibar wiki mbili zilizopita.
Dakika 45 za kwanza zilimalizika kukiwa hakuna timu iliyopata bao na kipindi cha pili na kipindi cha pili, John Bocco ‘Adebayor’ alianza kuifungia Tanzania kwa penalti dakika ya 53 kwa penalti.
Penalti hiyo ilitolewa baada ya beki wa Uganda kuunawa mpira uliopigwa na mshambuliaji wa Tanzania, Rashid Mandawa.
Uganda walifanikiwa kupata bao la kusawazisha dakika za lala salama kupitia Robert Sentongo baada ya mabeki wa Stars kutegeana kuondosha mpira na kwa matokeo hayo Uganda wanasonga mbele katika mbio za CHAN ya mwakani nchini Rwanda.
Kikosi cha Uganda kilikuwa; James Alitho, Denis Okot Oola, Brian Ochwo, Hassan Waswa Mawanda, Shafiq Bakari, Derick Tekkwo, Muzamil Mutyaba, Erisa Sekisambu, Farouk Miya, John Semazi na Robert Sentengo.
Tanzania; Ally Mustafa ‘Barthez’, Shomary Kapombe, Mwinyi Hajji Mngwali, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan, Mudathir Yahya, Deus Kaseke, Frank Domayo/Said Ndemla, John Bocco, Rashidi Mandawa na Simoni Msuva/Ramadhani Singano ‘Messi’.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni