Baada ya kujiunga na PSG kwa dau la paundi milioni 44, winga wa kimataifa wa Argentina, Angel di Maria amewaandikia barua ya wazi mashabiki wa klabu ya Manchester United ambayo ameichezea kwa mwaka mmoja.
Di
Maria alisajiliwa na Man United kutokea Real Madrid kwa ada ya paundi
milioni 60 na kuvunja rekodi ya usajili ya soka la England.
BARUA YA WAZI YA ANGEL DI MARIA KWA MASHABIKI WA MANCHESTER UNITED
"Naandika barua hii kuishukuru familia nzima ya Manchester United kwa kuniunga mkono kwa mwaka mmoja niliokuwa sehemu ya klabu.
Manchester
United waliponichagua kuwa sehemu ya timu yao, nilijisikia kuheshimiwa
kwasababu nilijua klabu hii ina maanisha nini na jinsi gani iliniamini.
Hata hivyo, nafahamu mambo hayakwenda vizuri kama tulivyotarajia, naomba msamaha kwa hilo.
Katika maisha ya mcheza mpira, kuna wakati mwingine mambo usiyotarajia na usiyoyataka yanatokea.
Nawahakikishia
kwamba haikuwa kujaribu. Nilijitahidi niwezavyo, lakini mpira sio kama
hesabu: Mara zote kuna vitu vingi vinavyoathiri vile unavyofikiria.
Samahani sana kwasababu sikufanya kile nilichotarajia katika klabu hii kubwa na ya ajabu.
Natoa
shukurani za pekee kwa bodi ya wakurugenzi na utawala ya Manchester
United, vilevile kila kiongozi na wachezaji wenzangu walioniunga mkono.
Pia shukurani za pekee ziwaendee mashabiki ambao mara zote waliniamini na kuonesha heshima na mapenzi makubwa.
Sasa ni wakati wa kujiunga na PSG, lakini Utukufu wa Manchester United utabaki kwenye kumbukumbu zangu daima.
Nawatakia kila la kheri
Angel di Maria".
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni