Nguli
wa Arsenal Thierry Henry anaamini kwamba Arsenal wanamhitaji Karim
Benzema ili waweze kutwaa taji la EPL na ligi ya mabingwa Ulaya.
Ingawa
Henry anahisi kwamba vijana hao wa Wenger hawako mbali na kufanya
maajabu, anaamini kwamba bado wanahitaji kuongeza nguvu katika kikosi
chao hasa safu ya ushambuliaji ili Giroud apate wa kusaididana naye.
"Mara zote nimekuwa nikisema kwamba huu ni mwaka wa Arsenal lakini kuna kitu cha kuongeza kwa sasa", alikaririrwa na talkSPORT.
"Nadhani kwa mwaka huu watapigania ubingwa endapo hawatokumbwa na majeraha ya hapa na pale.
"Ukiwa na Giroud kama mshambuliaji pekee – huwezi kushinda ligi, unahitaji mshambuliaji mwenye vionjo tofauti na Giroud.
"Nadhani
Giroud anafanya vizuri sana - alifunga magoli 14 ndani ya michezo 18,
hilo si jambo la mchezo - lakini wakati mwingine unahitaji mshambuliaji
mwenye vionjo tofauti na nahisi kama watampata Benzema, ghafla watakuwa
na nafasi kubwa ya kutwaa ndoo ya EPL na UCL".
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni