STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumatatu, 3 Agosti 2015

BERLUSCONI AKUBALI KUIUZA AC MILAN.

WAZIRI mkuu wa zamani wa Italia, Silvio Berlusconi amesaini makubaliano ya mauzo ya awali ya hisa asilimia 48 za klabu ya AC Milan kwa kundi linaloongozwa na mfanyabiashara wa Thailand Bee Taechaubol. 

Msemaji wa kampuni ya Fininvest inayomilikiwa na Berlusoni amesema mpaka ifikapo Septemba 30 mwaka huu hisa hizo zitakuwa zimehamishwa sambamba na malipo ya euro milioni 480. 

Klabu ya AC Milan inamilikiwa na Fininvest, kampuni inayomilikiwa na familia ya Berlusconi ambayo pia inamiliki kituo cha luninga cha Mediaset na kampuni ya uchapishaji ya Mondadori. 

Msemaji huyo amesema dili hilo limesainiwa na Fininvest na Taechaubol na kuthibitishwa na Berlusconi mwenyewe. 
Naye mfanyabiashara huyo wa Thailand alithibitisha taarifa hizo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram. 

Milan ambao ni mabingwa mara saba wa Ulaya, wamepoteza mng’aro wao katika miaka ya karibuni na kufanikiwa kushinda taji la mwisho la Serie A mwaka 2011. 

Klabu hiyo pia kwasasa inakabiliwa na madeni yanayofikia euro milioni 250 na mwaka jana wamepata hasara ya euro milioni 91.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox