MSHAMBULIAJI
kutoka Pape Abdoulaye N’daw kesho atafanyiwa mtihani wa kwanza wa
majaribio wakati Simba SC itakapomenyana na Mafunzo Uwanja wa Amaan,
Zanzibar.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe amesema kwamba
N’daw aliyetokea klabu ya Dinamo Bucuresti ya Ligi Kuu ya Romania
atacheza pia mechi nyingine Jumapili dhidi ya JKU.
“Baada
ya mechi hizo mbili, naamini benchi la Ufundi litakuwa limeona uwezo
wake na kuamua kama asajiliwe au aachwe aende,”amesema Kapteni huyo wa
zamani wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ).
Kuhusu
mchezaji kutoka Mali, Makan Dembele, Mwenyekiti huyo wa Kamati ya
Usajili ya Simba SC amesema kwamba anatarajiwa kuwasili leo. “Kumekuwa
na vikwazo katika safari yake, lakini tunadhani leo atafika,”amesema
kuhusu mchezaji huyo kutoka JS Kabylie ya Algeria.
Wawili
hao wanakuja baada ya Simba SC kuachana na Msenegali mwingine, Papa
Niang kufuatia kumjaribu kwa dakika 45 tu Jumamosi iliyopita katika
mchezo wa kirafiki dhidi ya Mwadui FC ya Shinyanga Uwanja wa Taifa, Dar
es Salaam timu hizo zikitoka 0-0.
Niang
alikuja Simba SC baada ya klabu hiyo kushindwa kufikia makubaliano na
mshambuliaji wa kimataifa wa Burundi, Kevin Ndayisenga juu ya dau la
usajili.
Niang
aliyetoka Alianza F.C. ya El Salvador ambaye ni mdogo wa mshambuliaji
wa kimataifa wa zamani wa Senegal, Mamadou Niang Jumamosi alishindwa
kabisa kuwashawishi wana Simba kwa soka yake duni.
Mchezaji
huyo wa zamani wa CF Mounana ya Gabon, Al Shabab SC ya Kuwait, FC
Vostok ya Kazakhstan, FF Jaro, AC Oulu na FC OPA za Finland aliondoka
usiku wa Jumamosi kurejea kwao, ikiwa ni baada ya siku tatu za kuwa Dar
es Salaam.
Awali
Simba SC pia ilishindwa kumsajili mshambuliaji mwingine hatari wa
Vital’O, Laudit Mavugo kufuatia klabu mbili za nchini humo kupandisha
thamani ya mchezaji huyo na kuwa Sh. Milioni 200, badala 110
walizokubaliana awali.
Aidha,
kuibuka pia kwa mzozo mpya kati ya klabu ya Vital’O FC na Solidarity
FC, inayodai kumlea Mavugo na kudai ina hakimiliki ya mchezaji huyo nako
kuliishitua Simba.
Vital’O
ikaikoroga zaidi Simba SC baada ya kudai kiwepo kipengele cha wao
kupata asilimia 50 kama mchezaji huyo atauzwa na Wekundu hao wa Msimbazi
kwenda klabu nyingine.
TANGAZA NASI: +255 655 442 255
CHANZI OPEN SCHOOL
Ijumaa, 28 Agosti 2015
Home
/
Unlabelled
/
HATMA YA MSENEGALI WA SIMBA SC KUJULIKANA KESHO, YULE DEMBELE WA MALI LABDA ATAWASILI LEO.....
HATMA YA MSENEGALI WA SIMBA SC KUJULIKANA KESHO, YULE DEMBELE WA MALI LABDA ATAWASILI LEO.....
About asantemuya
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA
Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni