WAKATI awali dirisha la usajili wa ligi lilikuwa lifungwe leo saa sita usiku, Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) limesogezwa mbele mpaka Agosti 20 mwaka huu.
Akizungumza na wandishi wa habari, Afisa Habari wa TFF, Baraka Kizuguto alisema dirisha la usajili wa wachezaji kwa Ligi Kuu Tanzania Bara, Ligi Daraja la Kwanza (FDL) na Ligi Daraja la Pili (SDL) sasa litafungwa Agosti 20 mwaka huu.
“Awali dirisha la usajili lilikua lifungwe leo , na usajili mdogo wa ndani ungefungwa Septemba 5, 2015 lakini sasa usajili wote kwa jumla utafungwa Agosti 20”, alisema Kizuguto.
Pia alisema Agosti Agosti 21- 28 ni kipindi cha pingamizi, Agosti 29-30 ,Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji itapitia na kupitisha usajili.
Dirisha la uhamisho wa wachezaji wa Kimataifa (FIFA –TMS) litafungwa Septemba, 6 na Ligi Kuu inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Septemba 12.
Aidha TFF inavitaka vilabu kukamilisha usajili huo katika muda uliowekwa, ili kupunguza usumbufu wa kufanya usajili dakika za mwisho,na dirisha litakapofungwa Agosti 20, litafunguliwa tena wakati wa dirisha dogo mwezi Novemba 15 mwaka huu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni