
Moja ya radha wanayoipata mashabiki wa Ligi soka nchini Marekani, MLS ni uhondo wa kuwatizama mastaa hawa waliotesa wakiwa barani ulaya sasa katika ligi yao.
Timu ya Frank Lampard, New York City Fc imesafiri hadi Los Angeles kuikabili LA Galaxy katika muendelezo wa ligi hiyo inayopata umaarufu wa kasi hivi sasa.
Kuelekea mechi hiyo ambayo New York inasafiri umbali mkubwa kiasi, hisia zimeanza kuteka mitazamo ya wadau mbalimbali wa soka kuhusu vita kati ya Gerard na Lampard waliopata kudumu katika klabu zao za Liverpool na Chelsea katika kipindi cha muongo mmoja uliopita.
Jumapili hii, mashabiki wa New York City Fc watawashuhudia nyota wao wakiongozwa na David Vila, Andrea Pirlo na Frank Lampard, huku wale wa LA Galaxy wakiwatazama kwa ukaribu, London Donovan, Steven Gerard na Robie Keane.
Mastaa hao ni moja ya kivutio kikubwa hivi sasa nchini Marekani, huku wakiongeza udhamini na hadhi ya ligi hiyo inayokua kwa kasi. Wachezaji hao, sanjari na kuonekana wameishiwa uwezo wa kupambana katika ligi soka za barani ulaya, lakini wanalipwa pesa nyingi sana katika ligi hii kuu nchini Marekani.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni