Thierry
Henry alikuwa gwiji la Arsenal, Walcott wakati akiwa mwokota mipira wa
Southampton, alitamani siku moja angalau kupiga naye picha.
Alifanikiwa
kufanya hivyo, siku alipojiunga na Arsenal. Alitamani kuwa kama yeye,
Henry alipoondoka, alikabidhiwa jezi yake namba 14.
Woga
ulimtawala akafikia kuomba namba 8, akaambiwa Samir Nasri anakwenda
kujiunga na Arsenal tayari kapewa jezi hiyo, baadaye akakubali kuivaa
namba 14.
Kumbuka, Walcott aliweza kuvuka, badala ya kupiga tu picha na Henry, akacheza timu moja pamoja naye.
Lakini
baadaye akawa mrithi wa jezi yake na Henry aliporejea Arsenal kwa mkopo,
safari hii Walcott ndiye alikuwa na jezi namba 14 na wakacheza timu
moja.
Jifunze kujiamini, kuwa na nia ya kutimiza ndoto yako lakini kujiamini kwenda mbali zaidi ya karibu unapotaka kufika.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni