STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumatatu, 3 Agosti 2015

MAMBO YA FEDHA: RONALDO AMNUNULIA WAKALA WAKE KISIWA KAMA ZAWADI YAKE YA HARUSI.

MSHAMBULIAJI nyota wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo amempa wakala wake Jorge Mendes kisiwa cha Greek kama zawadi katika harusi yake. 

Kisiwa hicho hakikutajwa jina lake lakini taarifa zinadai kuwa thamani yake inaweza kuwa zaidi ya euro milioni tatu. 

Taarifa kutoka nchini Hispania zinadai kuwa Ronaldo inavifahamu vyema visiwa vya Greek kwani amekuwa akivitumia mara kwa mara kwa mapumziko yake. 

Mendes alifunga ndoa na mpenzi wake wa siku nyingi Sandra nchini Ureno Jumapili iliyopita huku Sir Alex Ferguson akiwa miongoni mwa watu mashuhuri waliohudhuria harusi hiyo. 

Miongoni mwa watu wengine mashuhuri waliohudhuria sherehe hiyo ni pamoja na rais wa Real Madrid, Florentino Perez, rais wa benfica Luis Filipe Vieira na mmiliki wa klabu ya Chelsea Roman Abramovic.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox