STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumatatu, 3 Agosti 2015

JEZI MPYA ZA MAN UNITED ZALETA UTATA MKUBWA.

KAMPUNI kongwe ya vifaa vya michezo ya Adidas imetetea aina ya jezi mpya walizotoa kwa ajili ya timu ya wanawake ya Manchester United baada ya kukosolewa vikali kutokana na jinsi ilivyotengenezwa. 

Kampuni hiyo ya Ujerumani Julai mwaka jana walisaini mkataba wa miaka 10 wenye thamani ya paundi milioni 750 wakichukua nafasi ya kampuni ya Nike iliyomaliza muda wake. 

Lakini wakati wakitambulisha jezi mpya zitakazotumika kwa ajili ya msimu ujao wa 2015-2016, jezi za wanawake ambazo zenyewe zimewekewa shingo pana kulinganisha na wanaume zimekosolewa vikali na wadau mbalimbali wakidai zinaacha sehemu kubwa ya kifua nje. 

Lakini msemaji wa Adidas amesisitiza katika taarifa yao kuwa jezi hizo zimetengenezwa baada ya kupata ushauri kutoka kwa mashabiki huku asilimia 75 wakiunga mkono aina hiyo ya fulana.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox