STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumanne, 25 Agosti 2015

NYOTA SENEGAL AINGIA MATATANI UINGEREZA KWA KUTISHIA KUUA.

MCHEZAJI nyota wa kimataifa wa Senegal na klabu ya West Ham United, Diafra Sakho amekamatwa na polisi kufuatia tuhuma za kutishia kuua hadharani. Msemaji wa polisi alithibitisha kukamatwa kwa mshambuliaji huyo kwa tuhuma hizo na baadae kutolewa kwa dhamana. 

Naye msemaji wa nyota huyo alithibitisha taarifa hizo akidai kuwa Sakho amekanusha tuhuma hizo na wanasubiri uchunguzi wa polisi kabla ya kurejea tena polisi mapema mwezi Octoba. 

Sakho amekuwa akiandamwa na matukio ya nje ya uwanja katika siku za karibuni kwani mwezi uliopita alihojiwa na polisi kufuatia kuhisiwa kunyanyapaa. Sakho alijiunga na West Ham akitokea klabu ya Metz ya Ufaransa msimu uliopita na kufunga mabao 12 katika msimu wake wa kwanza Upton Park.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox