Shrikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limesaini mkataba mpya wa miaka mitatu
(3) wa udhamini wa ligi kuu Tanzania bara kuanzia msimu ujao na
mdhamini mkuu wa ligi hiyo ambayo ni kampuni ya simu za mkonnoni ya
Vodacom.
Katibu
mkuu wa TFF Selestine Mwesigwa amethibitisha kusainiwa kwa mkataba huo
lakini akasema hawakufanya sherehe za kutia saini mkataba huo kutokana
na mashindano ya Kagame yaliyokuwa yanaendelea nchini wakati TFF
ilikuwa ikiyasimamia kama shirikisho la soka la nchi mwenyeji.
“Kunakitu
wanasema katika ajira, unaposikia nafasi haijatangazwa na hajatangazwa
mtu mpya jua kwama kuna maendeleo na maranyingi ‘renewal’ ya ‘contract’
huwa hai-sound sana kama tunapoongelea mkataba ambao watu wameingia
udhamini mpya”, amesema Mwesigwa.
“Bila
shaka mdhami wa msimu wetu unaokuja ni Vodacom ambae tulikuwanae msimu
uliopita, kila kitu kimeshawekwa sawa ila kwa maana ya ceremony ndio
bado haijafanyika kwasababu kulikuwa na mambo mengi hapa katikati ya
Kagame na kadhalika”.
“Mkataba
ni miaka mitatu, kutakuwa na maongezeko ukizingatia kuna timu
zimeongezeka lakini nadhani hata kile kinachokwenda kwenye vilabu
kitaongezeka kwa kiasi fulani yako masuala mengi siwezi kuzungumza kwa
undani kwa sasahivi, kwa upande wa kwetu tulikuwa tunayaona hayapo
sawasawa. Kulikuwa na muda mwingi sana wakutosha kujadili karibu miezi
nane iliyopita kwahiyo kuna vitu vingi vimeangaliwa”.
Kwasababu
sherehe ya kusaini mkataba haijafanyika, sitaweza kuingia kiundani
zaidi lakini ni mkataba ulioboreshwa ukilinganisha na mikataba
iliyotangulia”.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni