Mlinda mlango mpya: Jenkinson akiondoa hatari langoni akiwa na jezi mpya kama golikipa
Carl
Jenkinson, ilimlazimu kucheza kama kipa jana katika mchezo kati ya West
Ham dhidi ya Leicester ambapo West Ham walipoteza mchezo huo kwa mabao
2-0, mchezo uliopigwa katika dimba la Upton Park, maskani kwa West Ham.
Wagonga
nyundo hao walikuwa wameshamaliza idadi ya wachezaji wao wanaotakiwa
kufanyiwa mabadiliko, na mbaya zaidi ni pale kipa wao Adrian alipopewa
kadi nyekundu na kumlazimu kutoka nje huku wakiwa hawaruhusiwa tena
kufanya mabadiliko.
Kipa wa West Ham Andrian akizawadiwa kadi nyekundu
Jenkinson akielekea langoni kuchukua mikoba ya Andrian
Hapo
ndipo mchezaji wa Arsenal anayecheza kwa mkopo katika klabu hiyo
Jenkinson, alipopelekwa langoni ili kuziba nafasi ya Andrian, na kufanya
vema kabisa akiwa langoni hapo.
"Nilihisi
kadi ile nyekundu ilikuwa kidogo ya kikatili, sawa alinyoosha mguu juu
lakini ilikuwa ni kwa bahati mbaya", alisema mchezaji huyo wa timu ya
taifa ya Uingereza U-21 baada ya mchezo.
"Ilinibidi nikakae mimi golini lakini nashukuru sikuwa na kazi kubwa sana ya kufanya maana sikupata rapsha nyingi".
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni