Picha ambazo zimekuwa zikizunguuka katika vyombo vya habari mbalimbali Uturuki zikimuonesha kiungo wa kimataifa wa Ujerumani anayeichezea klabu ya Arsenal ya Uingereza Mesut Ozil ameonekana akiwa na miss Uturuki kitu ambacho kinazua maswali mengi huenda wanamahusiano ya Kimapenzi.
Taarifa hizo zinakuja ikiwa masaa kadhaa yamepita toka beki wa zamani wa klabu ya Manchester United Gary Neville ahoji kuhusu mchango wa kiungo huyo katika klabu ya Arsenal ya Uingereza kabla ya mechi ya Liverpool dhidi ya Arsenal ambayo ilimalizika kwa 0-0.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni