|
|
Bayern Munich wametoa ofa ya paund 20 million kwa ajili ya kumnasa kinda wa kimataifa kutoka Italia anayekipiga kwenye timu ya Juventus Kingsley Coman, .
Source: Gazzetta dello Sport
Thursday, August 27, 2015 07:12
Thursday, August 27, 2015 07:12
|
|
Everton wanahitaji paundi 45m kwa ajili ya beki wao wa kati anayetakiwa kwa udi na uvumba na klabu ya Chelsea John Stones. Kocha wa timu hiyo Roberto Martinez amesema bado anamuhitaji kinda huyo ambaye ofa tatu za mwanzo za Chelsea zilikataliwa kwa mchezaji huyo.
Source: The Sun
Thursday, August 27, 2015 07:44
Thursday, August 27, 2015 07:44
|
|
Chelsea bado wanaimani ya kuwasajili wachezaji wawili kwa mpigo Paul Pogba na John Stones kabla ya dirisha la usajili kufungwa mwishoni mwa mwezi huu. Timu hiyo inajiandaa kutuma ofa mpya ya paundi milion 70 kwa ajili ya Pogba lakini bado wapo kwenye mazungumzo na Everton kuhusu Stones.
Source: Daily Mirror
Wednesday, August 26, 2015 22:37
Wednesday, August 26, 2015 22:37
|
|
Besiktas wamerudi tena kumtaka mchezaji wa kimataifa kutoka Nigeria ambaye anakipiga kunako timu ya Chelsea John Obi Mikel baada ya timu hiyo kushindwa kumpata kiungo kutoka Liverpool Lucas Leiva .
Source: Daily Mail
Thursday, August 27, 2015 00:07
Thursday, August 27, 2015 00:07
|
|
Manchester United wapo tayari kumuachia Jonny Evans kwa ada ya paundi milioni 12. West Brom na Everton zote zinavutiwa na huduma ya mchezaji huyu ambaye anatakiwa na Sunderland kwa muda mrefu.
Source: Daily Star
Wednesday, August 26, 2015 23:49
Wednesday, August 26, 2015 23:49
|
|
Juventus wanakaribia kumsajili kiungo wa kimataifa kutoka Cameron na klabu ya West Ham Alex Song.
Source: The Sun
Wednesday, August 26, 2015 23:18
Wednesday, August 26, 2015 23:18
|
|
Tottenham wanafikiria kuachana na mpango wa kumsajili mshambuliaji wa West Brom Saido Berahino kutokana na dau ambalo wameliweka mezani la paundi 21 kukataliwa na timu hiyo inayommiliki mchezaji huyo ikitaka paundi milion 25
Source: Daily Mail
Wednesday, August 26, 2015 22:57
Wednesday, August 26, 2015 22:57
|
|
Done Deal: Muda wowote kuanzia sasa Kevin De Bruyne ataondoka Wolfsburg na kujiunga na Manchester City.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni