Rias wa TFF Jamal Malinzi (kulia) akiwa na
Afisa Mtendaji Mkuuwa Azam Media, Rhys Torrington wakati wa makabidhiano ya mkataba wa kuanza michuano ya Ligi
Ya FA
SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu nchini (TFF) kwa kushirikiana na Azam Media, wameanzisha michuano ya Mpira wa miguuu itakayojulikana kwa “Azam Sports Federation Cup”.
Shindano hilo litatumia mfumo maarufu ambao unatumiwa nchini Uingereza katika michuano ya FA na vilevile nchini Uhispania katika michuano ya Copa del Rey .
Akizindua Shindano hilo jpya kabisa wakati wa hafla fupi iliyofanyika jijini Dar es Salaam na kushuhudiwa na viongozi mbali mbali wa Kampuni ya Azam Media na wamiliki wa timu za mpira nchini kutoka madaraja yote, Malinzi amesema michuano hiyo itazishirikisha timu 64 ambazo ni mjumuisho wa timu za Ligi Kuu, Ligi
daraja la kwanza na Ligi daraja la pili, timu itakayokwenda kucheza
ugenini itapewa Tsh milioni 3 kama gharama ya usafiri na itakayocheza
nyumbani itapewa Tsh milioni 1.
Malinzi amesema michuano hiyo itakuwa na msisimko mkubwa nchini na itakuwa huku lengo lake kubwa likiwa ni kuinua soka ambalo kimsingi limeshuka kutokana na ligi kuu kukosa timu nyingi.
Michuano hii itakuwa chachu katika kuleta msisimko wa Watanzania, hasa ukizingatia kwamba kwa kipindi kirefu wamekuwa wakitaka michuano kama hii ambayo inashirikisha timu za Ligi kuu pamoja na ligi daraja la kwanza na la pili ili kuleta hamasa katika mikoa ambayo haina timu inayoshiriki ligi kuu", alisema.
Malinzi ameongeza kuwa timu itakayochukua kombe hilo itajinyakulia kitita cha shilingi za Kitanzania milioni 50 pamoja na kupata nafasi ya kushiriki moja kwa moja kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika.
Amesema endapo timu ambayo ipo ligi kuu itashika nafasi ya 1 kwenye msimamo wa Ligi, na pia ikafanikiwa kuchukua kombe la FA basi nafasi hiyo itapewa na Timu ambayo itaingia fainali kwenye michuano ya FA.
Kwa Upande wake Afisa Mtendaji Mkuuwa Azam Media Rhys Torrington, amesema nia ya Kampuni yake kudhamini michuano hiyo ni kutaka kukuza mpira nchini kwa kutaka kufikia malengo.
Amesema licha ya kudhamini michuanao hiyo kwa kipindi cha Miaka 4, pia michuano hiyo itarushwa moja kwa moja kupitia Vituo vya TV vya Azam Media.
Udhamini utagharimu kiasi cha bilioni 3.3 kwa kila mwaka.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni