Alikuwa akiwindwa: Rais wa zamani wa Real Madrid Ramon Calderon amefichua kuwa walitaka kumchukua Wenger miaka ya nyuma.
Arsene Wenger, ilibaki kidogo tu kutua Real Madrid - na hayo yangekuwa ni mafanikio yake makubwa sana katika kazi yake ya ukocha.
Rais wa zamani wa Real Madrid Ramon Calderon, amefichua kwamba walitaka kumchukua Wenger miaka ya nyuma lakini alikataa na kuamua kubaki Arsenal.
"Yeyote ambaye anafanya kazi katika sekta yoyote ile angependa kubadilisha mazingira. Nadhani ni wazo zuri kuwa na kocha ambaye ana mipango ya muda mrefu kwenye timu.
“Tulikuwa tukiongea kuhusu Real Madrid na, kwa wakati ule, alikuwa akivutiwa sana na klabu lakini nini kilitokea.
Nakumbuka alisema: “Mnataka kwenda Hollywood tena, au kutengeneza timu ya soka?” Alimaanisha hivi mnataka kutengeneza filamu ya nyota wa Galacticos au kutengeza timu bora ya soka.
“Ni kitu kinachopatikana Uingereza ambacho ni kizuri sana kwa kweli. Kipo Arsenal, Manchester United pia, ambapo kocha anaweza kudumu klabuni kwa muda mrefu sana. Ni kitu kisichowezekana hapa.
“Nchini Uhispania, mashabiki na wafuasi wa Barcelona na Real Madrid, wanachohitaji wao ni ubingwa na makombe tu.
Lakini nchini Uingereza, ni kitu ambacho wanafanya vizuri sana –kumpa kocha sapoti na kumfanya najiamini. Kuweka uhusiano mzuri kati ya kocha na klabu. Wenger ni uthibitisho wa hilo.
“Kwa hiyo hatukuweza kufanikiwa kumleta na amependa sana maisha ya pale Arsenal… Wenger ... ni mtu mwenye heshima kubwa sana. huwezi kumkuta akibisha hovyo. Kuna baadhi ya nyakati ndio husikia akilaumu waamuzi lakini sio kama ambavyo Mourinho hufanya.
“Wenger ni mtu mwema sana. Ni kocha mwenye muonekano wa kipekee, mtu mzuri na ninafurahi sana kumuona akiwa amefanikiwa, lakini pia nadhani angekuwa mtu bora sana kwa klabu ya Madrid. Japokuwa Madrid ni klabu yenye ugumu wa aina yake wakati mwingine.
“Hebu ona yaliyomtokea Mourinho. alishinda kila kitu pale lakini. Pia kwa Capello… alipata mafanikio makubwa, lakini mashabiki hawakuwa na furaha na jini timu yao ilivyokuwa ikicheza na ndipo tulipolazimika kumtimua… Pia tatizo kama hilo lilikuwa kwa Mourinho.
“Arsene Wenger si aina ya makocha hao. Timu yake hupenda kucheza soka la kuvutia kwa mashabiki lakini pia kwa wadau wengine.
“Lakini hata hivyo tatizo bado ni hilo hilo tu. Ni vigumu sana kudumu na kocha kwa miaka hata mitatu tu. Presha huwa iko juu sana kutoka kwa mashabiki. Pia ni vigumu sana kuendana na presha ya vyombo vya habari.
“Ni hatari sana kama kocha haleti matokeo na hata kama akishinda basi hachezi mtindo ambao mashabiki hupendelea, hiyo inakuwa bado changamoto kubwa sana. Pengine angeweza kupata mafanikio, lakini kama unakuja hapa kuna mengi sana ya kuyatatua”.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni