Bondia Floyd Mayweather ni
jamaa mwenye rekodi nzuri ambayo ameijenga kwa kipindi chote cha miaka
yote 19 aliyoitumia kwenye mchezo wa ngumi..Usiku wa kuamkia leo
September 13 2015 kaiendeleza rekodi hiyo kwa kujiandikia ushindi mzuri
baada ya kumpiga Bondia Andre Berto… Baada ya hapo kuna kinachofuatia??
Stori ni nyingi kuhusu pambano lake na Manny Pacquiao kurudiwa, kuna stori kuhusu jamaa kuachana na mchezo wa Ngumi ‘Nimekamilisha kila kitu, nimefanya kila kitu kwenye mchezo wangu… Umri
wangu unakaribia miaka 40, hakuna nilichobakiza kwenye Ulimwengu wa
Ngumi, nahitaji kutumia muda mwingi zaidi na familia yangu‘ Hii ni moja ya nukuu ya alichokisema Floyd Mayweather baada ya pambano lake na Berto kuisha.
Baba yake Floyd anasema jamaa alilalamika sana maumivu ya mkono wakati akiendelea na pambano na Andre Berto, lakini hakuona kama ni tatizo kwa vile anaelekea kustaafu… Mayweather amemshinda Berto na kuandika headlines za ushindi wa 49 tangu alivyoanza mchezo wa Ngumi mwaka 1996.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni