Barcelona wamezoa Tuzo ya Klabu Bora Ulaya kwa Msimu wa 2014/15 iliyotolewa na Chama cha Klabu za Soka Ulaya, ECA(European Club Association).
Tuzo hiyo kwa Barcelona imekuja baada ya wao kutwaa Trebo, yaani Ubingwa wa La Liga, Copa del Rey na UEFA CHAMPIONS LIGI Msimu uliopita.
Sherehe za utoaji Tuzo zilifanyika Jana huko Geneva, Uswisi na Tuzo nyingine walitwaa Klabu ya Ukraine FC Dnipro Dnipropetrovsk waliopewa Tuzo ya Maendeleo Bora Mchezoni kwa kufika Fainali ya EUROPA LIGI bila kutarajiwa na kufungwa na Sevilla ya Spain.
Tuzo ya Ubora kwa Jamii na Programu Bora za Kijamii ilikwenda kwa Arsenal ambao wametambuliwa kwa mchango wao mkubwa kwa Jamii ya Jiji la London kukabiliana na tatizo la ajira kwa Vijana.
Tuzo ya 4 iliyotolewa na ECA ni ile ya Mafanikio Bora ambayo ilibebwa na Klabu ya Estonia Levadia Tallinn kwa mpango wao uitwao 'Pamoja Tutasonga' ambao ulilenga kusaidia Walemavu wanaohitaji msaada wa kuongozwa na Mbwa ili kuingia kirahisi Uwanjani kwa ajili ya Mechi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni