TIMU
ya Inter Milan imewafunga mahasimu AC Milan 1-0 na kupanda kileleni mwa
Serie A jana, huku mshambuliaji Mario Balotelli akikosa mabao ya wazi
baada ya kutokea benchi kucheza dhidi ya timu yake ya zamani, The
Rossoneri.
Fredy
Guarin alisherehekea mechi yake ya 100 ya ligi kwa kufunga bao pekee la
ushindi dakika ya 58 baada ya kupoteza nafasi kadhaa.
Balotelli,
ambaye ambaye amerejea Milan kwa mkopo kutoka Liverpool mwezi uliopita
aligongesha mwamba na baadaye akakaribia kufunga kwa mpira wa adhabu,
kabla ya kuzinguana na Filipe Melo wa Inter.
Balotelli
alianzia Inter kabla ya kuhamia Manchester City mwaka 2010 na jana
alitokea benchi kwenda kucheza dhidi ya timu iliyomuibua ambayo
mashabiki wake walimzomea jana.
Kikosi
cha Inter Milan kilikuwa; Handanovic, Santon, Medel, Murillo, Nunes
Jesus/Telles dk68, Guarin, Felipe Melo, Kondogbia, Perisic/Ranocchia
dk85, Icardi na Jovetic/Palacio dk72.
Ac
Milan; Lopez, Abate, Zapata, Romagnoli, De Sciglio, Kucka/Poli dk72,
Montolivo, Bonaventura, Honda/Cerci dk81, Luiz Adriano na
Bacca/Balotelli dk62.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni