Uingereza imefanikiwa kuingiza mamilioni ya fedha kwa mwaka jana tu na
kujiongeza kiuchumi kupitia soka.
Watalii
wanaofikia 800,000 kutoka nje yaUingereza wametembelea nchini hiyo kwenye
viwanja mbalimbali vya mpira wa miguu na kuisaidia Uingereza kuingiza pauni
milioni 684.
Fedha
hizo ni zaidi ya zile ambazo Tanzania huingiza kupitia utalii hapa nchini.
Uwanja
unaomilikiwa na Manchester United wa Old Trafford wenyewe ndiyo umetembelewa
zaidi sawa na ule wa Emirates wa Arsenal. Kila mmoja umetembelewa na watalii
109,000.
Pamoja
na kuyumba katika ligi, lakini watalii 99,000 walitembelea Anfield wa Liverpool
na Chelsea ikapanda kwa kupata watalii 89,000 kupitia Stamford Brigde.
Hii
inaonyesha kiasi gani mchezo wa soka ukiendelezwa unavyoweza kugeuka na kuwa
kitegauchumi kwa watu binafsi lakini hata serikali.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni