Kocha wa Manchester United Louis van Gaal alijiunga na klabu ya Man United toka mwaka 2014 akichukua mikoba ya David Moyes aliyetimuliwa kazi.
Imeripotiwa kuwa Van Gaal sio kocha rafiki na wachezaji, kitu kilichopelekea kumkosa Pedro Rodriguez.
September 10 stori iliyofichuka ni kuwa Louis van Gaal aligombana na wachezaji toka msimu wa Ligi Kuu haujaanza, stori kutoka mtandao mirror.co.uk unaeleza kuwa kikubwa kilichopelekea Van Gaal
kupishana na wachezaji wake, ni aina ya mfumo anaotumia kuwasliliana na
wachezaji sio rafiki, hivyo kujikuta akigombana na wachezaji kutokana
na ukali wake.
Stori inasema kuwa wakati timu ipo Marekani kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya, Van Gaal
aliwakataza wachezaji kutembea, wala kufanya kitu chochote kwa madai
kuwa kilichowapeleka ni maandalizi ya msimu na sio kingine chochote.
Hivyo wachezaji wakawa na ratiba ya kula, kufanya mazoezi na kulala.
Kocha Louis van Gaal
sio rafiki wa wachezaji inadaiwa mastaa wengi wa klabu hiyo wamewahi
kutofautiana na kocha huyo.
Wachambuzi wa masuala ya soka wanasema kwa
ushirikiano huu ni ngumu kupata mafanikio akiwa na wachezaji ambao hana
mahusiano nao mazuri.
Di Maria amewahi kukiri moja kati ya sababu zilizomfanya ahame Man United ni Van Gaal.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni