Hatimaye timu ya taifa ya England maarufu kama Simba watatu ‘three lions’ imefuzu kucheza michuano ya ulaya ‘EURO 2016′ nchini Ufaransa mara baada ya kufikisha points 21 katika kundi lake jana usiku.
England walifikisha points hizo baada ya kuwafunga vibonde San Marino kwa mvua ya magoli 6-0 katika mechi iliyochezwa nyumbani kwa San Marino ambao wanashika mkia katika kundi lao.
England sasa watacheza mechi nyingine siku ya Jumanne dhidi ya Switzerland katika uwanja wa Wembley katika kile kitakachokuwa kutimiza ratiba ya michezo iliyosalia.
Lakini sanjari na hayo, kitu kilicholeta mvuto wa kipekee ni goli alilofunga nahodha Wayne Rooney ambalo kimsingi limemuweka katika magoli sawa na Sir Bob Charlton ya ufungaji bora wa muda wote wa nchi hiyo baada ya kufikisha magoli 49 huku wote wakiwa wamecheza michezo 106.
Bado Rooney ana nafasi ya kuandika historia mpya ya ufungaji kutokana na ukweli kwamba bado ana michezo mingi zaidi ya kucheza siku za usoni. Watu watafurika katika uwanja wa Wembley Jumanne hii kuona kama Rooney anaandika historia yake.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni