5. Radamel Falcao. Kutoka AS Monaco kwenda Chelsea.
Alikuwa na msimu mbovu
alipokuwa Manchester United msimu uliopita licha ya kupewa nafasi kubwa
ya kucheza. Aliishia kufunga mabao manne tu. Lakini Mourinho ameamua
kumleta vivyo hivyo akiamini ataisaidia timu yake.
4. Papy Djilobodji. Pauni milioni 2.2
Kutoka Nantes kwenda Chelsea.
Ripoti mbalimbali kutoka nchini
Ufaransa zinaeleza kuwa hakuna chochote ambacho beki huyo anaweza
kuwapa Chelsea. Iliripotiwa kuwa alitaka kupelekwa katika vilabu
mbalimbali vya Uingereza lakini alikataliwa licha ya bei yake kuwa
ndogo. Kwa uwezo uwanjani wataalamu wanasema hana kiwango cha kuwashinda
Zouma,Cahill au mlinzi mwingine yeyote wa Chelsea.
3. Fabian Delph. Kutoka Aston Villa kwenda Manchester City.
Mwanandinga huyu hana uwezo wa kuwashinda Yaya Toure,
Silva,Fernadihno, Navas,Fernando, Sterling,Debruyne na hata Nasri, ndio
maana mpaka sasa tunaweza kusema kuwa hana nafasi ya kucheza katika
kikosi cha kwanza kwa City.
2. Younes Kaboul. Kutoka Tottenham Hotspur kwenda Sunderland.
Sunderland walikuwa na tatizo
kubwa katika safu ya ulinzi msimu uliopita. Waliruhusu magoli mengi sana
ambayo yangeweza kuwasababisha kushuka daraja. John Oshea na Wes Brown
kwa sasa wakati umeshaanza kuwatupa mkono, Sasa usajili wa Kaboul mwenye
miaka 29, ambaye pia ni ni mwepesi wa kuapata majeraha ya mara kwa mara
ni tatizo jingine.
1. Bastian Schweinsteiger – Euro milioni 14. Kutoka Bayern Munich kwenda Manchester United.
Bastian Schweinsteiger anaweza
kuwa moja ya wachezaji wenye uzoefu mkubwa katika klabu ya Manchester
United kwa msimu huu, lakini sio wa kucheza katika kikosi cha kwnza kwa
dakika zote . Kwa sasa Bastian ana umri wa miaka 30. Mechi dhidi ya
Swansea na Newcastle zilithibitisha hilo. Badala yake Bayern Munich
waliamua kumsajili Arturo Vidal kuziba pengo lake, Vidal ni mchezaji
ambaye United walikuwa wakihusishwa naye wakatika wa dirisha la usajili
la mwezi January.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni