Ndio maana sio suala la kushangaa ama kuuliza kwa nini Cristiano Ronaldo aliamua kutumia akaunti yake ya Twitter kuitangaza kampuni moja ya ushonaji ya nchini Ureno, vile vile kwa nini Wayne Rooney aliamua kuposti picha ya Nike katika viatu vya kuchezea mpira wa gofu?
Jibu
ni kwamba, hela ndio chanzo ya hayo yote. Utafiti unaonesha kwamba
wachezaji kama Ronaldo, Rooney na Neymar wanaweza kupata maelfu ya pauni
kwa tweet moja tu kutoka kwa baadhi ya wadhamini wao wakubwa
ulimwenguni.
Orodha
hii ya wachezaji wenye thamani kubwa katika mtandao wa Twitter, si tu
kwa wanandinga bali pia hata kwa wachezaji wa michezo mingine kama vile
staa wa NBA LeBron James na Kevin Durant ambao wote kwa pamoja wanaingia
kwenye orodha hii.
Ronaldo inasemekana amejikusanyika kiasi cha pauni 169,280 kwa tweet yake dhidi ya bidhaa ya Nike.
Hii ndio orodha ya mastaa mbalimbali wa michezo ulimwenguni wanaoongoza kwa kunufaika na mtandao wa Twitter.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni